BURUDANI:Belle 9 amemkosea Sana Madee, anatakiwa achapwe fimbo 70 – Dogo Janja

Mwezi Juni 7, 2018 msanii wa muziki kutoka Moro Town, Belle 9 akihojiwa na kituo cha Radio cha Jembe FM cha jijini Mwanza alimtaja Madee kama rapa wa Tanzania ambaye haelewi nyimbo zake kabisa anaona kama mzugaji kwani anaona ni msanii ambaye anatoa ‘beat’ tu na sio wimbo
Rejea maneno ya Belle 9 kwenye mahojiano hayo “Honesty, let me be honesty, Madee huwa simuelewi. I don’t know, ujue kuna wasanii inafika kipindi unasikiliza unasema huyo mtu ana-release beat sio wimbo tena, Labda kwa vile nasikiliza rappers ambao wanajua sana au kuna kitu nakitegemea kutoka kwake kutokana muda mrefu yupo kwenye game, kuna kitu nakimisi, so naona kama nikimsiliza na lose,”.

Sasa kufuatia kauli hiyo, Dogo Janja amemjia juu Belle 9 kwa kumwambia kuwa amekosea sana kumbeza msanii mkongwe kama Madee ambaye ameshawahi kutoa ngoma kali nyingi hata kabla ya Belle 9 kujulikana kwenye muziki.
Dogo Janja akizungumza kwenye kipindi cha eNEWS cha EATV amesema kuwa Belle 9 amekosea na hana budi kupigwa fimbo 70 hadharani kwa kitendo hicho cha kumvunjia heshima Madee.
Kitu cha kwanza hata yeye Belle 9 kuna vitu anafanya kuna watu huwa hawamuelewe, hata mimi mwenyewe kuna wanangu kibao huwa wananiambia bora Nuruely. Alichokifanya Made kwenye muziki, Belle 9 hata robo hajafikia.. Respect a legend, waheshimu wakongwe, waheshimu wazee sio busara kutukana wakongwe,“amesema Dogo Janja na kusisitiza.
Kakosea amemkosea mzee, anatakiwa apigwe 70 bomani (wamasai hapo wamenielewa) ukivunja sheria au ukimkosea mkubwa au mzee unatakiwa uchapwe fimbo 70 mbele ya wanabomani wote.. Madee mpole sana ndio maana wanamuonea. ni mkongwe anayezeeka na heshima zake,“amesema Dogo Janja.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAHAMU: Nchi zenye wanaume wenye maumbile makubwa duniani Congo yawa tishio

FAHAMU: Nchi za Afrika zenye warembo matata zaidi Je Tanzania ipo?