Mwezi Juni 7, 2018 msanii wa muziki kutoka Moro Town, Belle 9 akihojiwa na kituo cha Radio cha Jembe FM cha jijini Mwanza alimtaja Madee kama rapa wa Tanzania ambaye haelewi nyimbo zake kabisa anaona kama mzugaji kwani anaona ni msanii ambaye anatoa ‘beat’ tu na sio wimbo Rejea maneno ya Belle 9 kwenye mahojiano hayo “ Honesty, let me be honesty, Madee huwa simuelewi. I don’t know, ujue kuna wasanii inafika kipindi unasikiliza unasema huyo mtu ana-release beat sio wimbo tena, Labda kwa vile nasikiliza rappers ambao wanajua sana au kuna kitu nakitegemea kutoka kwake kutokana muda mrefu yupo kwenye game, kuna kitu nakimisi, so naona kama nikimsiliza na lose, ”. Sasa kufuatia kauli hiyo, Dogo Janja amemjia juu Belle 9 kwa kumwambia kuwa amekosea sana kumbeza msanii mkongwe kama Madee ambaye ameshawahi kutoa ngoma kali nyingi hata kabla ya Belle 9 kujulikana kwenye muziki. Dogo Janja akizungumza kwenye kipindi cha eNEWS cha EATV amesema kuwa Belle 9 amekosea na hana budi kupigwa ...