MICHEZO: Gor Mahia Ya kenya Kiulaini Ndani Ya Goodson Park, Ni Mara Baada Ya kumla Mnyama Mapema Jana
Mechi ya fainali ya SportPesa Super Cup imemalizika kwa mabingwa wa Ligi Kuu nchini Kenya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Afraha mjini Nakuru, Gor Mahia walitawala zaidi mchezo wakiwa na kikosi chao kamili huku Simba wakipata wakati mgumu kutengeneza nafasi za kufunga.
Gor Mahia wamejipatia mabao yao kupitia kwa Mshambuliaji wao hatari, Medy Kagere aliyefunga la kwanza katika dakika ya 6 tu ya mchezo na kufanya kipindi cha kwanza kiende kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili kilianza tena kwa Gor Mahia kuzidi kulisakama lango la Simba wakionesha njaa ya kupata goli jingine ambapo mnamo dakika ya 54, Tuyisenga alifunga bao la pili kwa kumalizia mpira wa krosi uliopigwa kutoka kulia mwa Uwanja na kumuacha Kipa Aishi Manula akiwa hana cha kufanya.

Maoni
Chapisha Maoni